Beki wa kulia klabu bingwa nchini Italia Juventus FC Dani Alves, amewatoa hofu mashabiki wake ambao walikumbwa na wasiwasi kuhusu dhoruba iliyompata akiwa katika mchezo wa ligi hapo jana dhidi ya Genoa.

Alves alipata majeraha ya mguu na kutolewa nje ya uwanja kwa msaada wa watu wa huduma ya kwanza, hali ambayo ilizua hofu kwa viongozi wa benchi la ufundi, wachezaji wenzake pamoja  na kwa mashabiki.

Mara baada ya mchezo huo, beki huyo mwenye umri wa miaka 33 aliandika katika ukurasa wa mtandao wa Instagram, ambapo alieleza maendeleo ya afya yake.

Aliandika: “Nashukuru kwa ujumbe mlionitumia wa kunitakia pole, lakini niwahakikishieni kwamba nipo salama na sikuvunjika kama ilivyokua inadhaniwa, japo ninakabiliwa na maumivu makali.

“Nipende kuwafahamisha kuwa, famia na jamaa zangu wote wapo sambamba na mimi, na wamethibitisha sikuumia kwa kiasi kikubwa.

“Nitarejea uwanjani siku kadhaa zijazo, na nina uhakika nitakua fit zaidi ya ilivyokua katika michezo kadhaa niliyocheza tangu mwanzoni mwa msimu huu.”

Alves ambaye ameshacheza michezo minane ya ligi akiwa na Juventus FC, alipata maumivu ya mguu baada ya kuchezewa hovyo na Lucas Ocampos wakati wakiwania mpira.

Katika mchezo dhidi ya Genoa mabingwa wa Sirie A (Juventus FC) walipoteza mchezo kwa kukubalia kufungwa mabao matatu kwa moja.

Mpina: Wanaotubeza wamekosa hoja za msingi
Wilhelm Gidabuday Katibu Mkuu RT