Beki na nahodha wa klabu bingwa nchini Hispania Real Madrid Sergio Ramos amemtahadharisha rais wa klabu hiyo Florentino Perez, kufuatia mpango wa usajili wa kiungo wa Real Betis Dani Ceballos.

Cebbalos ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaounda kikosi cha Hispania chini ya umri wa miaka 21, anatarajiwa kusajiliwa na Real Madrid baada ya mchezo wa fainali wa michuano ya Ulaya dhidi ya Ujerumani unaochezwa leo.

Perez na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane, wamekubaliana kufanya usajili wa kinda huyo, ili awe mbadala wa kiungo Luka Modric, licha ya kutarajia kubakishwa kwa mkopo Real Betis.

Tovuti ya Diario Gol imeeleza kuwa, Ramos amemtahadharisha Perez juma hili kwa kumwambia kwamba, kuna haja akajiridhisha kwa kina kuhusu usajili wa kiungo huyo ambaye anaamini ana mapenzi na FC Barcelona.

Ramos alimueleza kiongozi huyo kwamba, mara kadhaa amekua akimfuatilia Ceballos katika akaunti zake za mitandao ya kijamii, na ameoona mchezaji huyo ana mapenzi na FC Barcelona, hivyo ana wasiwasi huenda akashindwa kuwajibika ipasavyo kama atasajiliwa Estadio Santiago Bernabeu.

Malinzi akubali yaishe, aachia ngazi TFF
Video: Diamond alivyoliamsha, akizindua Diamond Karanga