Shirikisho la soka nchini Gabon FEGAFOOT, limemtangaza aliyekua nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Daniel Cousin, kuwa kocha mkuu.

Maamuzi ya shirikisho la soka nchini humo, yemakuja kufuatia baba wa mshambuliaji wa klabu ya Arsenal ya England Pierre-Emerick Aubameyang (Pierre-Francois Aubameyang), kukataa uteuzi wa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gabon.

Katika uteuzi wa awali Cousin alikua ametajwa kama msaidizi wa Pierre-Francois Aubameyang, na sasa amepandishwa cheo na kuwa kocha mkuu, ambaye anakabiliwa na mtihani wa kuivusha Gabon hadi kwenye fainali za Afrika za mwaka 2019, zitakazofanyika nchini Cameroon.

Cousin mwenye umri wa miaka 41, amewahi kucheza soka akiwa na klabu za Hull City ya England, Rangers ya Scotland, na Lens ya Ufaransa.

Image result for Pierre-Francois AubameyangPierre-Francois Aubameyang

“Amekubali uteuzi tulioufanya kwa mara ya pili, kuanzia leo Daniel Cousin atakua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gabon.” Imeeleza taarifa ya shiriksiho la soka nchini Gabon (FEGAFOOT), na kuthibitishwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC.

Cousin, ambaye aliichezea timu ya taifa ya Gabon katika michezo 56 na amewahi kuwa meneja timu hiyo (The Panthers) tangu mwaka 2014, amesema: “Nikiwa kama nahodha wa zamani wa timu hii, nitahakikisha ninatumia ujuzi na maafira yangu katika harakati za kukijenga kikosi imara. Nitahakikisha ndoto za mashabiki wa soka wa Gabon zinakua kweli.”

Kikosi cha Gabon kilikua kinanolewa na kocha kutoka nchini Hispania Jose Antonio Camacho, ambaye alishindwa kusaini mkataba mpya, baada ya kuzungumza na viongozi wa FEGAFOOT, kabla ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zambia mwezi huu.

Katika mchezo huo kikosi cha Gabon kilikubali kupoteza kwa kufungwa bao moja kwa sifuri.

The Panthers watacheza dhidi ya Sudan Kusini mara mbili mfululizo mwezi ujao, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON 2019).

Nafasi za ajira kutoka makampuni 11 Tanzania
China yalitambua rasmi kanisa katoliki

Comments

comments