Kiungo wa Chelsea, Danny Drinkwater amejiunga na Kasimpasa ya Super Lig huko Uturuki kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, baada ya kukabiliwa na changamoto ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha franka Lampard.

kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 hajacheza kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea kwa miaka miwili na nusu, huku mara ya mwisho alionekana akiwa amevalia uzi wa Blue Agosti 2018.

Amecheza mara 23 kwa Miamba hiyo ya London Magharibi, lakini ni tangu walipopoteza Ngao ya Jamii mbele ya Manchester City mnamo 2018 alipotokea benchi.

Drinkwater amewahi kutolewa kwa mkopo kwenye klabu za Burnley na Aston Villa Msimu uliopita, msimu huu alijiunga na wachezaji wa chini ya miaka 21 na chini ya miaka 23 wa Chelsea, ili kukidhi hajaya kucheza angalau kila mwishoni mwa juma.

Drinkwater ambaye bado ana mkataba wa miezi 18 huko Stamford Bridge, alieichezea England mara tatu, aliisaidia Leicester City kushinda taji la Ligi mnamo 2015-16, lakini ameshindwa kutamba akiwa na Chelsea ajiunge nao kwa pauni milioni 35 mnamo 2017.

Kipindi Akiwa kwa Mkopo huko Burnley na Aston Villa Msimu uliopita hakuwa na nafasi, akiwa amecheza mara mbili tu kwa Clarets na mara nne kwa Villians, ndipo msimu huu alipoichezea timu ya Chelsea chini ya umri wa miaka 21 kwenye Mashindano ya Papa John’s Trophy na chini ya miaka 23 katika mechi za Premier League 2.

Tanzania, Uingereza 'pasu kwa pasu' mkataba wa madini
JKT yasitisha mafunzo