Klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani ipo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu ya Tottenham, kwa ajili ya kufanikisha usajili wa mkopo wa beki wa pembeni kutoka England Danny Rose.

Wakati mazungumzo ya pande hizo mbili yakiendelea, taarifa zinaeleza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa biashara ya usajili wa beki huyo ikafanikiwa kutokana na hitaji lake la kutaka kucheza mara kwa mara.

Taarifa ziliziotolewa usiku wa kuamkia leo na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha England, mchezaji huyo ameshapewa ruhusa na kuzungumza na viongozi wa Schalke, ili kufanya makubaliano binafsi na uongozi wa klabu hiyo.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Spurs walitangaza kuwaweka sokoni baadhi ya wachezaji wake ambao ni Toby Alderweireld, Mousa Dembele, pamoja na Rose, kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza, huku wakihitaji kucheza mara kwa mara.

Rose mwenye umri wa miaka 28, kwa muda mrefu amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kuihama klabu hiyo, kwa kusudio la kutaka kupata changamoto mpya ya soka lake, hasa baada ya kukosa nafasi ya kudumu kwenye kiksoi cha kwanza cha Spurs.

Suala lingine ambalo linamsababishia beki huyo kufikiria kuondoka klabuni hapo, ni sakata la kuponda mfumo wa malipo ya mishahara kwa wachezaji wa Spurs, ambapo mwaka 2017 aliwahi kusema mfumo huo umeweka matabaka baina yao, lakini baadae aliomba radhi kwa kutoa kauli hiyo.

Msimu uliopita Rose alicheza michezo 10 pekee ya ligi kuu ya soka nchini England.

Jack Grealish kubaki Aston Villa
Video: Mkapa asononeka, Zitto, Matiko wapigwa mabomu

Comments

comments