Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ameendelea kuingia majaribuni kuhusu kikosi chake ambacho kitakwenda kushiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 (Euro 2016) huko nchini Ufaransa mwezi ujao.

Hodgson, ameendelea kuwa katika majaribu kufuatia mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck kupata maumivu wa goti wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Man City uliochezwa jana kwenye uwanja wa Etihad.

Welbeck, alishindwa kuendelea na mchezo huo, baada ya kugongwa sehemu za goti na beki wa pembeni wa Man City Bacary Sagna, na alipopatiwa matibabu alijaribu kujikongoja uwanjani lakini ilishindikana.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, anatarajia kufanyia vipimo hii leo, ambavyo vitatoa majibu ya mustakabali wake, kama atakuwa sehemu ya kikosi cha England ama la.

Tayari Hodgosn ameshahakikishiwa kumkosa kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain ambaye anakabiliwa na maumivu ya goti ambayo yaliibuka tena baada ya kujitonesha akiwa katika mchezo wa kikosi cha akiba.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson anatarajia kutangaza kikosi chake May 13 na atawasilisha orodha ya mwisho ya kikosi hicho huko UEFA Juni 2 tayari kwa fainali za matafaifa ya barani Ulaya.

Riyad Mahrez Akata Mzizi Wa Fitna, Asema Kinachofuata
Young Africans Kukabidhiwa Mwali Wao Mjini Mtwara