Hofu imetanda Emirates Stadium kufuatia jeraha linalomkabili mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Danny Welbeck, ambaye jana alishindwa kumaliza mchezo wa mkondo wanne hatua ya makundi ya Europa League dhidi ya Sporting Lisbon.

Mshambuliaji huyo alilazimika kutolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu, alipokua kwenye harakati za kutaka kupiga kichwa kuelekea langoni mwa timu pinzani na alipoanguka alifikia mguu wake wa kulia.

Meneja wa Arsenal Unai Emery, aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana, Welbeck alikimbizwa hospitali moja kwa moja, na walikua wanasubiri majibu ya vipimo.

“Alikimbizwa hospitali moja kwa moja, hatujapata taarifa zozote kuhusu majibu ya vipimo alivyofanyiwa, lakini inavyoonekana alipata majeraha makubwa kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia,” Alisema boss wa Arsenal Unai Emery.

Image result for Danny Welbeck injuryDanny Welbeck akitolewa nje ya uwanja kwa machela

“Kila jeraha lina tofauti, huenda kawa amevunjika ana kuteuka, lakini bado majibu ya vipimo atakavyofanyiwa yatatoa picha kamili ya jambo nitakalowaeleza baadae.”

“Alipaswa kuwa nasi hapa, lakini kutokuwepo kwake kunadhihirisha ana tatizo mkubwa, ninawasihi muwe na subira taarifa za mchezaji huyu zitatolewa.”

Welbeck mwenye umri wa miaka 27, alipatwa na majeraha hayo katika dakika ya 25, na ilimchukua muda kupewa huduma ya kwanza akiwa uwanjani huku akisaidiwa kupumua na mashine ya hewa safi (Oxygen).

Roberto Soldado na wenziwe waadhibiwa Uturuki
Bailly atajwa kikosi cha Ivory Coast