Mshambuliaji Danny Welbeck huenda akarejea tena uwanjani mwishoni mwa mwaka huu, kufuatia jeraha lake la goti alilolipata mwezi May mwaka huu kuendelea vizuri.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, alithibitisha taarifa za mshambuliaji huyo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikosi chake kuelekea katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa ligi ya nchini England, ambao utawakutanisha na mabingwa watetezi Leicester City.

Wenger alisema Welbeck anaendelea vyema na alipokea taarifa kutoka kwa matabibu wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London na wamemthibitishia uwezekano wa mshambuliaji huyo kurejea uwanjani wakati wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Welbeck alipatwa na majeraha ya goti alipokua katika mchezo wa ligi ya England dhidi ya Man City na alitarajiwa kurejea uwanjani baada ya miezi tisa, kufuatia upasuaji mdogo aliofanyiwa siku chache zilizofuata.

Jose Mourinho Kumbembeleza Zlatan Ibrahimovic
Video: Kuna watu wanaona ukuu wa idara ndiyo kila kitu - Waziri Mkuu