Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck huenda akawa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita, baada ya vipimo alivyofanyiwa jana kuonyesha alipatwa na matatizo makubwa katika goti la mguu wake wa kulia wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Man City.

Welbeck, alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England, kwa ajili ya fainali za barani Ulaya (Euro 2016) alipatwa na mejeraha ya goti, baada ya kugongwa na beki wa pembeni wa Man City, Bacary Sagna.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, atakuwa na bahati mbaya ya kupata majeraha ya goti, kwani alifanikiwa kurejea uwanjani mwezi februari mwaka huu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita ambayo alikua akijiuguza jeraha kama hilo.

Kukosekena kwake kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita ijayo, kutakua pigo kubwa kwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson kutokana na kuonyesha hitaji la kuwa na Welbeck katika fainali za barani Ulaya ambazo zitaanza rasmi mwezi ujao huko nchini Ufaransa.

KAMPUNI YA KIJAPAN KUWEKEZA KWENYE UMEME
John Terry Awekwa Njia Panda, Mkataba Wake Kumalizika Mwezi Ujao