Ngoma maarufu ya wacheza dansi wa jamii ya Gule Wamkulu wa nchini Zimbabwe, imezusha taharuki baada ya jamii kugawanyika juu ya uhalali wake kwamba imekuwa ya siri na yenye kufuata matambiko ikiambatana na vurugu, hali iliyopelekea waratibu wa tamasha hilo la Gule Mkuu jijini Harare kufikiria kuliondoa.

Kwa mujibu wa mratibu wa Tamasha hilo, Notice Mazura amesema wahusika husherehekea kumbukumbu za wazee walioleta utamaduni huo kutoka nchi ya Malawi lakini watu huona tamaduni hizo ni za watu wasioweza kufikiri na wasiosoma.

Onesho la Nyau Dansi nchini Zimbabwe. Picha ya Anadolu.

Kutokana na mizozo hiyo, sifa ya jamii husika tayari imeharibika nchini Zimbabwe kutokana na kuongezeka kwa vikundi vya wanaokopi ngoma hizo na hatimaye kuzusha vurugu na kufanya uhalifu wa unyang’anyi, wizi, unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji.

Kiongozi wa shirika la Gule Wamkulu, Kennedy Kachuruka amesema ni muhimu kutofautisha kati ya watendaji wa kweli na wacheza densi wa kuiga kwani wengi wao huzunguka na silaha na ni wahalifu wenye ujeuri ambao huwashambulia watu wasiopenda tamaduni hiyo.

Washiriki wa Nyau Dansi wakipita mtaani jijini Harare. Picha ya AP.

Amesema, “Mwonekano wa Gule Wamukulu na wakati mwingine tabia za wacheza Nyau ndio huwafanya watu wafikirie kuwa wanaweza kuwa wakorofi au wamejihusisha na mambo mengine, watu hawa wanajua dawa nyingi za asili kama zile zingine.”

Asili ya ngoma hiyo inaweza kufuatiliwa hadi karne ya 17 ambapo ilihusishwa na watu wa Chewa wanaozunguka nchi za Malawi, Zambia na zile za kusini mwa Afrika.

Kelvin Mandla amrithi Sbai Karim Simba SC
Mabadiliko hali ya hewa chanzo vifo watu 600