Katika kuhakikisha vitendo vya ushoga vinakwisha kabisa nchini kwa kuwa ni kinyume na vitabu vya dini pamoja  na maadili ya kiafrika Waziri wa Afya jinsia walemavu na watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali imepiga marufuku vilainishi kwani ndivyo vinavyovhochea  vitendo hivyo.

Mh. Mwalimu amesema kuwa kuruhusu kuendelea kuwepo kwa vilainishi hivo ni kuruhusu vitendo vya ushoga ambavyo vinasababisha ongezeko la Ugonjwa wa Ukimwi huku akitaja mikoa ya Dar es saalam na Dodoma ndio inayoongoza kwa kuwa na watu wengi wanaofanya  vitendo hivyo.

Hata hivo ameongeza kwamba wadau mbali mbali wanaungana na serikali katika kuhakikisha vilainishi hivyo wanavikusanywa na kuteketezwa.

”tunashukuru kwa sasa wadau wengi wameshaanza kujitokeza na wamekubaliana na agizo la kutouza, tayari wameshaanza kuvikusanya kwa ajili ya kuviteketeza”

Aidha waziri huyo amesema kwa sasa serikali inajikita katika sekta ya afya na kujenga wodi ya wazazi ili kuimarisha sekta ya afya.

”Kipaumbele cha serikali ni kujenga wodi za kina mama pamoja na kununua madawa hospitalini na siyo kutoa hela kwa ajili ya vilainishi vya makundi hayo”. Alisema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa makundi hayo yapo hatarini kwa kiasi kikubwa kupata maambukizi ya vvu kutokana na kujihusisha na vitendo hivyo kwa kasi zaidi.

 

Watu Wanajaribu Kutengeneza Bifu Kati yangu na Diamond- Chameleone
Kanuni Za Ligi Kuu Zamuondoa Tom Olaba Ruvu Shooting