Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha zinaweza kuwa nzito na hatari katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani wiki hii.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ikiijumuisha pia Pemba na Unguja visiwani Zanzibar. Kwa mujibu wa TMA, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kwa wingi kuanzia Aprili 13 hadi 16 mwaka huu. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za mfululizo na zitazidi kipimo cha mililita 50 ndani ya saa 24 huku zikiwa na wastani wa asilimia 70.

TMA imeeleza kuwa hali hiyo ya mvua kubwa inatokana na kuimarika kwa unda wa mvua sambamba na uwepo wa kimbunga kiitwacho Fantala katika ukanda wa Bahari ya Hindi.

Wakazi wa maeneo hayo wametakiwa kuchukua tahadhari kadri iwezekanavyo.

Ralph Krueger: Ronald Koeman Haondoki Southampton
Anne Kilango afananisha yaliyomsibu na ‘Msiba’