Mkoa wa Dar es salaam, umekuwa kinara katika uandikishaji wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakao fanyika Novemba 24 nwaka huu, baada ya kuandikisha kwa asilimia 89 hadi kufikia siku ya jumatano huku mikoa ya Kigoma na Kilimanjaro ikivuta mkia kwa kuwa na asilimia ndogo.

Akitoa taarifa hiyo, jana Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo amesema baada ya kuongezwa kwa muda, shughuli imeenda vizuri kwani mikoa yote imejiandikisha juu ya asilimia 50.

Mastaa 3 wanaolipwa pesa ndefu zaidi na Instagram

Waziri Jafo amewanyooshea kidole watendaji katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kwakuwa halmashauri pekee ambayo bado uandikishaji wake upo chini ya asilimia 50.

Amesema hadi kufikia Oktoba 15, watu milioni 16.9 ambayo ni sawa na asilimia 74 walikuwa wamesha jiandikisha hivyo zoezi linaenda vizuri kwani wakuu wa mikoa na wilaya wameamua kufanya kazi.

Asilimia 25 ya mazao Duniani yanaathiriwa na sumukuvu

Waziri Jafo ametaja mikoa ambayo inaongoza  ni Dar es salaam(89), Pwani (86), Tanga (81), Mtwara (80) na Lindi asilimia (77), na kwa upande wa mikoa ya chini ni Kigoma (57), Kilimanjaro (58), Arusha (66) na shinyanga asilimia 66.

Beyonce ashika nafasi ya pili mwanamke mwenye mvuto zaidi duniani
Mastaa 3 wanaolipwa pesa ndefu zaidi na Instagram