Fainali za 21 za Kombe Dunia zinatarajiwa kuanza Juni 14 mwaka huu nchini Urusi na kufikia tamati Julai 15, kwa kushirikisha mataifa 32 yaliyofuzu kucheza fainali hizo.

Mataifa 31 yalifuzu kupitia hatua za mpambano mkali katika kanda zao ambazo ni Afrika, Ulaya, Asia, Oceania, Amerika ya Kati na Kaskazini pamoja na Amerika ya kusini, huku Urusi wakiingia kama wenyeji.

Mataifa hayo baada ya kufuzu kucheza fainali hizo, yalipangwa katika makundi manane tofauti, katika hafla maalum iliyofanyika Disemba Mosi mwaka jana.

Kutoka barani Asia, timu zilizofuzu zipo tano (5): Australia, Iran, Japan, Saudi Arabia na Korea Kusini.

Bara la Afrika litawakilishwa na timu tano (5): Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia.

Amerika ya kati na kaskazini (CONCACAF) itawakilishwa na timu tatu (3); Costa Rica, Mexico na Panama

Amerika ya kusini (CONMEBOL) itawakilishwa na timu tano (5): Argentina, Brazil, Colombia, Peru na Uruguay

Bara la Ulaya, itawakilishwa na timu kumi na nne (14) ambazo ni Ubelgiji, Croatia, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani (Mabingwa watetezi), Iceland, Poland, Ureno, Urusi (Wenyeji), Serbia, Hispania, Sweden na Uswiz.

Fainali za kombe la dunia za mwaka huu 2018, zitakuwa za kwanza kuchezwa barani Ulaya tangu mwaka 2006, ambapo Ujerumani walikuwa wenyeji, na timu ya taifa ya Italia ilitwaa ubingwa.

Zitakuwa fainali za kwanza kufanyika Ulaya ya Mashariki, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930.

Urusi imejiandaa kikamilifu kuhodhi fainali hizo na tayari wameshatangaza viwanja vitakavyotumika.

Viwanja vilivyoandaliwa kwa ajili ya fainali hizo ni vipo katika miji ya Kaliningrad, Kazan, Krasnodar, Moscow, Nizhny Novgorod, Rostov-on-Don, Saint Petersburg, Samara, Saransk, Sochi, Volgograd, Yaroslavl, na Yekaterinburg.

Dar24.com imeakuandalia kwa kifupi uchambuzi wa timu zote 32, kuelekea fainali za kombe la dunia 2018. Kila siku, tutakuwa makala hapa kukuchambulia timu moja, uifahamu mapema kabla kipyenga hakijapulizwa.

Aidha, kupitia channel yetu ya YouTube, tutaendelea kukupa historia ya ‘makubwa’ yaliyojili katika fainali hizi tangu kuanzishwa kwake.

‘Kuwa karibu na Dar 24, uwe karibu na Urusi’.

Mwambie rafiki amwambie rafiki.

Video: Alikiba awataka watanzania wasione haya kuitwa waswahili
BOT Yaziunganisha benki ya Twiga na Benki ya TPB