Mtandao wa Dar24 unatarajia kuzindua app mpya ya simu za Androids (programu ya simu za kisasa), Desemba 31 mwaka huu ikiwa ni zawadi kwa watanzania katika kuufunga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.

Uongozi wa Da24 umeeleza kuwa App hiyo itawarahisishia watu wote wanaomiliki simu za Androids kupata taarifa katika mfumo wa habari za kuchapishwa/kuandikwa, habari kwa njia ya sauti pamoja na video kwa haraka zaidi na katika mfumo uliorahisishwa zaidi.

App hiyo itapatiakana kwenye ‘Google Play Store’ kwa jina la ‘Dar24’.

“Siku zote huwa tunafanya kazi na kufikiria namna ya kuwahudumia kwa ufanisi zaidi watu wote kwa kuzingatia mahitaji yao ya kupata taarifa za habari, habari mpasuko, vichekesho, masimulizi na mambo mengine kwa wakati na kwa urahisi,” Umesema Uongozi wa Dar24 kwenye taarifa yake.

“Tunaimani hii app itakuwa rafiki zaidi na bora zaidi kwa watumiaji wa Androids wanapotafuta huduma ya msingi. Tunawashukuru watu wote kwa kutuunga mkono katika huduma zetu wakati wote katika mtandao wetu wa www.dar24.com , ukurasa wetu wa facebook, twitter na Instagram. Sasa tunaongeza App bora zaidi ya Dar24 ambayo tunauhakika wataipenda,” inaeleza taarifa hiyo.

Filamu Mpya ya Star Wars aliyoigiza Lupita Nyong'o yavunja Rekodi Za Mauzo, Angalia Trailer Hapa
Marufuku uvaaji Vimini, Mlegezo