Daraja refu la juu ‘flyover’ katika jiji la Kolkata (Calcutta) nchini India jana limeporomoka na kuua takribani watu 23 kuwajeruhi wengine 100.

Tukio hilo baya liemetoka katika eneo la Girish Park, sehemu ambayo inadaiwa kuwa na idadi kubwa ya wakaazi wanaoishi katika nyumba zilizokaa kimsongamano.

Picha zilizopikwa usiku wa tukio hilo zinaonesha wenyeji wa eneo hilo wakijaribu kuwaokoa kwa mikono wahenga huku watu wengine wengi wakidaiwa kunasa kwenye daraja hilo.

Daraja hilo lenye urefu wa Kilometa 2 lilikuwa katika hatua za matengenezo tangu mwaka 2009 na lilikuwa likishindwa kukamilika kwa muda uliopangwa kwa mara kadhaa.

Hata hivyo, bado sababu za kutokea kwa tukio hilo hazijawekwa wazi lakini Kampuni iliyokuwa ikijihusisha na ujenzi wa daraja hilo imeahidi kushirikiana na maofisa wanaofanya uchunguzi kubaini chanzo.

CCM yaeleza yatoa tamko kuhusu Wabunge wao wanaotuhumiwa Kwa Rushwa
Mke afariki kwa mshtuko baada ya mumewe 'kutumbuliwa jipu' na Kasi ya Magufuli akipenyeza tumbili