Serikali kupitia msemaji mkuu wa Serikali imesema ujenzi daraja la mto Wami na barabara zake umefikia asilimia 70.4.

Katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema daraja hilo litakamilika Novemba 21, 2022.

Amesema daraja Lina urefu wa meta 510 na gharama ya ujenzi ni Bilioni 67.7.

Aidha amewapongeza wakala wa barabara TANROADS kwa kazi hiyo.

Daraja la mto Wami lilianza kujengwa mwaka 2018 kwa gharama za serikali za zaidi ya shilingi Bilioni 67 na lilitarajiwa kukamilika kwa miezi 24.

Shiboub, Tenana kukiwasha Mapinduzi CUP 2022
Ahemd Ally: Ni uzito wa dunia nzima