Darassa amevunja ukimya kuhusu mjadala uliowasha moto mwishoni mwa mwaka jana baada ya mchambuzi mmoja wa muziki kumtaja kuwa ndiye mwana ‘Hip Hop bora wa mwaka 2016’.

Mtazamo huo uliibua vuguvugu la mabishano makali kati ya waliounga mkono na waliupinga kwa nguvu kwenye mitandao ya kijamii.

Kundi hilo la waliompinga likiongozwa na Mwana hip hop mkongwe na anayeheshimika kwa vina na jumbe ‘conscious’, Nash MC lilieleza kuwa Darassa hastahili kuwa katika orodha ya wana hip hop kwa kuwa tayari ameshabadili mtindo wake kwa alichofanya kwenye ‘Muziki’.

Darassa amefunguka kupitia kipindi cha Ladha 3600 cha E-FM kinachoongozwa na Jabir Saleh, akieleza kujiepusha na mijadala ya mitazamo ya watu wanaoupinga muziki wake na badala yake anajikita katika kuwatumikia wanaoukubali muziki wake.

“Mimi kwa upeo wangu mdogo sana, sina comment ya kum-judge au kum-push mtu ambaye anasema mimi ni ‘No’. Cha kufanya nina plan za ku-deal na wale ambao wanasema ‘Yes’ kwa muziki wangu,” Darassa alifunguka.

“Nitafanya kazi kwa ajili yao, kazi ambayo wao watachagua kusema Darassa kafanya nini. Lakini nitafanya muziki mzuri. Kwa sababu mwisho wa siku, mabishano yetu na majigambo yetu hayaijengi nchi… ndio maana nasema acha maneno weka muziki,” aliongeza.

Hata hivyo, rapa huyo alieleza kuwa anaheshimu pia wazo la mtu ambaye amejiamini kupinga kile ambacho watu wengi wanakikubali kwani hajui chanzo cha ujasiri na msimamo wake.

‘Muziki’ umekuwa wimbo mkubwa zaidi wa hip hop kwa mwaka 2016 na pia wimbo wa msanii wa hip hop ambao kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi umeweza kuzifunika hata nyimbo kubwa za wasanii wa kuimba.

Wimbo wake umeendelea kutikisa kwa kasi mitandao ya kijamii na kuangaliwa kwa kasi YouTube, na sasa umeanza kuvuka mipaka ya Tanzania.

Trump aigeuka Urusi sakata la udukuzi wa mitandao, aipa 'za uso'
Video: Mjema agawa vyandarua Ilala, asisitiza wananchi wazingatie matumizi yake

Comments

comments