Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Mabasi ya Mwendo Kasi (DART), imetakiwa kubuni mikakati ya kuboresha huduma ya usafiri huo na kuongeza wigo wa huduma katika maeneo yanayokidhi vigezo ikiwemo jiji la Dodoma, Mbeya, Arusha, Mwanza na Tanga.

Rai hiyo, imetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi), Angellah Kairuki na kusema mikakati hiyo pia isaidie kutoa huduma nchi nzima.

Mabasi ya Mwendo kasi jijini Dar es Salaam.

Amesema, uanzishwaji wa Wakala huo ulikuwa ni maalum kwa Jiji la Dar es salaam lakini kwasasa upo uhitaji kwa Majiji mengine ambayo yanakidhi vigezo vya kupata huduma ya mabasi ya mwendo kasi.

Kuhusu, hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Kairuki ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha zinajibiwa kwa wakati na kwamba hatarajii kupata homa zinazojirudia.

Nelson Okwa aenguliwa Simba SC, Chama arejea
Juma Mgunda: Tupo tayari kuivaa Ruvu Shooting