Mipango ya mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid ya kutaka kumsajili beki wa kulia kutoka nchini Austria na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani David Alaba, huenda ikashindikana kufuatia mchezji huyo kusisitiza kupendezwa na mazingira ya mjini Minich.

Real Madrid waliibua hisia za kutaka kumsajili Alaba tangu miezi miwili iliyopita lakini kumekua hakuna muendelezo wa suala hilo.

Alaba alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Bayern Munich mwezi March mwaka huu ambao utafikia kikomo mwaka 2021.

“Ninafurahia kucheza hapa na ninatarajia kuendelea kuwa hapa, na ndio maana nilikubali kusaini mkataba mpya wa kucheza FC Bayern Munich, Amesema Alaba alipokua akihojiwa na jarida la BILD.

“Carlo Ancelotti anafahamu ni vipi ninachokihisi hapa, najiona nipo nyumbani, na meneja amenihakikishia kwamba ninaweza kucheza kwa mipango aliyokujanayo.”

 

England Kujipima Kwa Mabingwa Wa Dunia Wa 2010
Lamine Kone Aomba Kuondoka Stadium Of Light