Mustakabali wa Mlinda Lango wa Manchester United, David de Gea, hadi sasa haujulikani kwa sababu taarifa zinaeleza huenda akatimka klabuni hapo katika dirisha hili kubwa.

Kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu baina ya klabu na Mlinda Lango huyo juu ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mashetani wekundu hao. Lakini De Gea hadi sasa hajakubaliana na Manchester United juu ya ofa ambayo amemwekewa mezani.

Taarifa za ndani zinaeleza Mlinda Lango huyo aliyeitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu amepiga chini ofa ya mkataba mpya.

Huku sababu zikielezwa ni maslahi ambayo yapo kwenye mkataba huo mpya na hayajampendeza golikipa huyo kwani anahitajika kupunguza mshahara wake ili kusalia klabuni hapo.

Dea Gea ndio mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya United, hivyo kupewa ofa ya mkataba mpya ambayo itamhitaji kupunguza maslahi yake ni kitu ambacho inaelezwa hajakubaliana nacho kabisa.

Kuondoka kwa De Gea pia kunasababishwa na kubadilika kwa mpira kwani timu nyingi zinahitaji golikipa wa kisasa ambaye anaweza kucheza kuanzia nyuma na kupiga pasi kwa usahihi, kitu ambacho Mhispania huyo hakiwezi na Kocha Ten Hag, mara kadhaa amezungumza juu ya kuhitaji golikipa mwenye uwezo wa kucheza kuanzia nyuma na mwenye ufanisi katika kupiga pasi.

Paulo Dybala, Mourinho njia panda AS Roma
Wabunge watakaopinga harakati za rais kukiona