Wachezaji  wawili wa Manchester United, David de Gea na Chris Smalling wameng’ara katika tuzo za msimu za klabu hiyo inayofundishwa na Louis van Gaal.
De Gea ameshinda tuzio ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la mashabiki wa klabu, wakati Smalling ameshinda Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la wachezaji wenzake katika sherehe zilizofanyika usiku wa Jumatatu Old Trafford.
Smalling poses with girlfriend Sam Cooke on a memorable night for the defenderSmalling said it was a huge honour to join some of the star names who have won Players' Player in the past Chris Smalling kushoto akiwa na mopenzi wake na kulia akiwa amebeba tuzo ya mchezaji bora wa mwaka chaguo la wachezaji wenzake
Kipa wa kimataifa wa Hispania, De Gea amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu akiokoa michomo mingi ya hatari na kuisaidia United kubeba pointi.
Mshambuliaji kinda, Marcus Rashford ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa umri chini ya miaka 18, wakati beki Cameron Borthwick-Jackson ameshinda Mchezaji Bora kwa vijana chini ya umri wa miaka 21.
Rufaa Ya Geita Gold Sports Yagonga Mwamba TFF
Hii hapa Siri ya Marekani kutoonesha picha za mwili wa Osama Baada ya kumuua