Mahakama Kuu kanda ya Tabora, leo imetoa maamuzi yake juu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafufulila (NCCR-Mageuzi) dhidi ya Husna Mwilima (CCM).

Mahakama hiyo imehalalisha ushindi wa Mwilima na kutupilia mbali maombi ya Kafulila ya kumvua ubunge kada huyo wa CCM kwa madai kuwa alimpora ushindi wake.

Katika kesi hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari, ilivuta usikivu wa wananchi wengi jimboni humo na Tanzania kwa ujumla.

Wafuasi wa CCM wakisherehekea ushindi wa Mwilima

Wafuasi wa CCM wakisherehekea ushindi wa Mwilima

Kafulila aliungana na Mawakili wake, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera huku Mwilima akitetewa na wakili Kenedy Fungamtama na mawakili wa Serikali.

 

AVEVA: TUNAOMBA RADHI
Mabingwa Watetezi Nao Wataja Kikosi, Manguli Waachwa

Comments

comments