Aliyekua meneja wa klabu ya Man Utd, David Moyes amekataa kurejea nchini Engalnd, baada ya kuombwa na viongozi wa klabu ya Sunderland ambao wanahaha kumsaka mbadala wa Dirk Nicolaas “Dick” Advocaat aliyetangaza kujiuzulu mwishoni mwa juma lililopita.

Gazeti za Sportsmail, limebaini kuwepo kwa mazunguzo kati ya viongozi wa The Black Cats, dhidi ya Moyes kwa kipindi cha siku kadhaa na waliamini huenda meneja angekubali ombi lao.

Lakini pamoja na kuweka msimamo wa kubaki nchini Hispania anapofanya kazi kwa sasa kwenye klabu ya Real Sociedad, David Moyes, alituma muwakilishi wake ambaye ni Jimmy Lumsden kwenda nchini England kutazama mazingira ya klabu ya Sunderland.

Jibu alilolipata inasemekana halikumridhisha na badala yake amemua kuendelea kubali katika ligi ya nchini Hispania (La Liga) ambayo amekua huko tangu mwaka 2014.

Sunderland, walifuata utaratibu wa kutaka kuvunja mkataba wa Moyes kwa kuzungumza kwanza na viongozi wa klabu ya Real Sociedad, na walipewa nafasi ya kuendelea na mchakato wao lakini muhusika ameshaonyesha dhamira ya kutotaka kurejea nchini England.

Baada ya David Moyes kukataa kurejea England, uongozi wa klabu ya Sunderland unaendelea na mchakato wa kumsaka mbadala wa Advocaat, kwa kuelekeza nguvu zao kwa aliyekua meneja wa klabu ya Burnley, Sean Dyche pamoja na Sam Allardyce aliyeachana na West Ham Utd mwishoni mwa msimu lililopita.

Sir Alex Ferguson Aendelea Kutetea Uamuzi Wake
Liverpool Yaonyesha Dhahir Mapenzi Kwa Klopp