Hatimae uongozi wa klabu ya Sunderland umemaliza fununu za kuondoka kwa beki wao kutoka nchini Ivory Coast Lamine Kone, baada ya kumsainisha mkataba mpya ambao utamuweka Stadium of Light hadi mwaka 2021.

Kone alisajiliwa na klabu ya Sunderland mwezi Januari mwaka huu akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia Lorient, na alianza kuibua hisia za kutaka kuihama klabu hiyo kufutia ombi aliloliwasilishawakati wa usajili wa majira ya kiangazi ya kutaka auzwe kutokana na meneja mpya David Moyes kushindwa kumuonyesha ushirikiano wa kutosha.

Hali hiyo ilizua taharuki kwa kwa watu wake wa karibu na kufikia hatua ya kumini huenda asingekuwepo katika mipango ya Moyes, ambaye alichukua nafasi ya Sam Allardyce miezi mitatu iliyopita.

Klabu ya Everton ilionyesha nia ya kumsajili Kone, lakini David Moyes alikua kikwazo kwa kukataa ofa iliyotumwa Stadium of Light na badala yake alimuhakikishia nafasi katika kikosi chake cha kwanza beki huyo mwenye umri wa miaka 27.

“Lamine ni mchezaji muhimu katika mipango yangu na nilifanya kila njia ili asiondoke wakati wa majira ya kiangazi

“Ni mchezaji pekee ambaye amecheza katika kikosi cha Sunderland tangu mwezi januari na ameonyesha kuyamudu mazingira ya soka la England.” Tovuti ya klabu ya Sunderland imemnukuu Moyes.

 

Barack Obama ni kati ya watoto waliolelewa na mzazi mmoja, nini chanzo cha malezo hayo?
JPM amuapisha Dk. Dau kuwa Balozi wa Tanzania Malaysia