Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Nigeria David Adeleji Adeleke maarufu Davido, ameingia kwenye vichwa vya habari kwa taarifa ya kustaajabisha baada ya kutoonekana kwenye shughuli ya mazishi ya aliyekuwa mpiga picha wake maalum.

Fortunate Ateumunname Peter ambaye alifariki dunia siku ya jumanne septemba 21 mwaka huu baada ya kuzama mtoni huko Lekki, Lagos amezikwa na watu wachache katika mazishi yaliyohusisha ndugu wa karibu pekee mjini Lagos Nigeria.

Licha ya marehemu kuwa mtu waliyefanya naye kazi kwa ukaribu na kwa kipindi kirefu mpaka hatua ya mwisho ya uhai wake timu nzima ya Davido hawakuhudhuria mazishi hayo.

Mashabiki na wadau mbali mbali hasa walio karibu na familia ya marehemu wamekaririwa wakimshutumu msanii Davido kwa kutoonekana katika tukio la mazishi hayo.

Kumbukumbu pekee inayotajwa kuhusu Davido juu ya kifo cha Fortune ni post yake aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram septemba 25, 2021 ambapo alidhihirisha kusikitishwa sana na kifo cha mpiga picha wake huyo na kubainisha kuwa amempoteza mtu muhimu, mfanya kazi hodari na mwenye kujituma na kuwa kifo chake kimemuachia majonzi na pengo lisiloweza kuzibika.

Inaelezwa kuwa chanzo cha kifo cha Fortune kilitokana na kusombwa na maji na kisha kuzama katika kina kirefu wakati akijaribu kutafuta kupiga picha bora karibu na eneo la mto wenye kina kirefu uliopo Lekki mjini Lagos Nigeria.

Mtanzania ashinda Nobel
Majaliwa agoma kufungua barabara