Msanii wa muziki nchini Nigeria, Davido ameweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa na mpenzi wake Chioma aliyepata umaarufu mara baada ya kuzawadiwa gari la kifahari katika siku yake ya kuzaliwa mwaka jana.

Davido ametumia ukurasa wake wa Twitter kutoa taarifa hiyo mara baada ya mashabiki wake kumhoji kuhusu malengo yake na mwanadada huyo alioamua kuweka wazi juu ya mahusiano yao.

Davido alipohojiwa juu ya kufunga ndoa na Chioma  hakuchukua muda kujibu swali hilo na kusema kwa sasa huo ndio mpango wake kufunga ndoa na mwanadada huyo.

Hata hivyo siku chache zilizopita  Chioma aliamua kufuta picha zote na kuufuta ukurasa wake wa instagram bila kutoa sababu ya kufanya maamuzi hayo hali ambayo ilileta tafsiri tofauti kwa mashabiki wakidhani kuwa wawili hao tayari wamefarakana.

Aidha, kwa hapa Tanzania tunaona msanii anayemake headline kwenye suala na ndoa ni Diamond Platinumz ambaye amekuwa akipiga kalenda mashabiki wake ambao kwa hamu wanasubiri siku ya harusi yake kufika na huku wengine wakidai kuwa suala la Diamond kuoa ni ndoto ya Alinacha, kwani ni jambo ambalo haliwezi kutokea hivi karibuni kutokana na sababu wanazozifahamu wao.

Nini maoni yako tuandike hapo chini.

LIVE: Rais Magufuli akipokea ndege nyingine ya Tanzania
Bastola bandia yawaponza wanne watiwa mbaroni

Comments

comments