Baada ya mwaka mmoja kupita rapa maarufu nchini Marekani, J cole ametangaza kurejea kwa tamasha lake kubwa linalofahamika kama DreamvilleFestival amabalo mwaka jana halikufanyika na kutangaza majina  ya mastaa watakao tumbuiza katika tamasha hilo

Tamasha hilo litafanyika April 6 mwaka huu huko North Carolina ambapo mwaka jana halikufanyika kutokana na athari ya kimbuka kiitwacho, Hurricane Florence ambacho kilisabaabisha madhara makubwa katika maeneo ya North Carolina na kufanya tamasha hilo lisifanyike

Aidha, rapa huyo ametoa orodha ya mastaa watakao tumbuiza katika tamasha hilo huku mwanamziki maarufu kutoka Nigeria, Davido akitarajiwa kupanda jukwaa moja na mastaa kama 21 Savage, Big Sean, SZA, Teyana Taylor, 6LACK, Pamoja na Nelly ambapo tiketi za tamasha hilo zimeanza kuuzwa

Hata hivyo,Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Dorothea Dix Park in Raleigh, North Carolina kama heshima kwa mashabiki wake ambao walikumbwa na maafa ya kimbunga mwaka jana na kuahirisha tamasha hilo na kulifanya tena mwaka huu kwa kufuta kiu ya mashabiki wake.

Bavicha walalama, ' Tuacheni tushindane kwa hoja'
Video: Majaliwa atua Koromije, 'Tumeamua kuiboresha na kuipandisha hadhi'

Comments

comments