Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza waganga Wakuu wa Mikoa kuwakamata wote wanaouza dawa zinazoeleza kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu za kiume ambazo hazijasajiliwa na mamlaka husika.

Hayo yamezungumzwa leo bungeni pindi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji ambae aliibua mada ikihusu tatizo la wanaume wengi kukosa nguvu za kiume na kuhoji serikali kama inaufahamu na tatizo hilo ambalo limekuwa chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika.

Mada hiyo iliibua mzozo Bungeni na kuwafanya wabunge wengi kutaka kuchangia hoja kuhusiana na tatizo hilo.

Khatib Haji ameendelea kuihoji serikali kuwa  endapo inatambua uwepo wa tatizo hilo, imechukua  hatua gani kukabiliana na tatizo hilo na kwa nini Tanzania imekuwa ya 10 duniani miongoni mwa nchi zilizopoteza furaha,” ameuliza Khatibu Haji.

Pia swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Dk. Hamsi  Kigwangalla ambapo alikabiliana na swali hilo kwa kusema kuwa Serikali inatambua wazi tatizo hilo ijapokuwa hakuna jibu la moja kwa moja kwa kuwa tendo la ndoa ni tendo la siri.

Na ameweka bayana  baadhi ya visababishi vya wanaume wengi kukosa nguvu za kiume zikiwemo, umri mkubwa zaidi ya miaka 60, kifua kikuu, kisukari, ukimwi na wanaotumia dawa muda mrefu.

 

Simba na Yanga sasa kucheza Azam Complex
Wapigaji vichwa 11 vya treni kukiona