Bingwa wa Olyimpiki marathoni katika mbio za masafa marefu upande wa wanawake, Mkenya Jemima Sumgong, amepigwa marufuku kutoshiriki shindano lolote la riadha kwa muda wa miaka minne baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli zinazokatazwa michezoni.

Sumgong ni mwanariadha wa pili wa ngazi ya juu mwanamke kupata adhabu kama hiyo, baada ya bingwa wa mbio za New York na Boston Rita Cheptoo kupigwa marufuku pia.

Shirikisho la riadha nchini Kenya-AK, limesema Sumgong ataanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu wakati aliposimamishwa kwa muda.

Sumgong ndiye mwanariadha wa Kwanza wa Kenya kushinda medali ya dhahabu katika mbio za marathoni za Olyimpiki.

Meek Mill ahukumiwa kwenda jela miaka 2-4
Kesi mbili za kupinga matokeo zafunguliwa Kenya