Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka jijini Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kutekeleza zoezi la usajili na utoaji wa vibali kwa magari ya kusambaza majisafi (water Bowsers) katika jiji la Dar es Salaam na Pwani.
 
Zoezi hilo la Usajili litaendeshwa kwa wiki mbili kuanzia Mei 15 litadumu kwa wiki mbili mpaka Mei 29, 2019 eneo la kituo cha Chuo Kikuu cha Ardhi yenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal, Tegeta na Bagamoyo.
 
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Afisa Mawasiliano wa DAWASA, Joseph Mkonyi wakati akisimamia zoezi hilo, ambapo amesema kuwa zoezi hilo linalengo la kuwatambua wauzaji wote wa majisafi ikiwa na kuangalia usalama wa vyombo wanavyotumia kuwauzia maji wananchi.
 
”Niwaombe wote wenye kufanyabiashara ya majisafi kujitokeza ili tuweze kuwatambua na kuwapa leseni na kuwapa mikakati yenye lengo la kujenga ili watoe huduma salama,”amesema Mkonyi.
 
Aidha, zoezi hilo la usajili linamtaka mwenye gari kuja na vielelezo ikiwemo picha moja ya rangi ya mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA au HATI YA KUSAFIRIA). Kingine ni Nakala ya kasi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya dereva vyote viwe vimethibitishwa na mwanasheria.
 
Hata hivyo, ameongeza kuwa matenki yatakayokuwa yamekidhi vigezo vya kupata usajili yatasafishwa na dawa maalumu ya kuua wadudu kwenye mantenki na kubandikwa stika ya DAWASA.

Video: Fahamu utamaduni wa kuhudumia maiti kama mtu aliye hai
LIVE: YANAYOJIRI BUNGENI DODOMA LEO MEI 16, 2019