Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kuimarisha miundombinu na miradi mikubwa ikiwemo wa Mabwepande na kuwashukuru wananchi kwa uvumilivu wa kipindi mgao wa maji ambao amesema kwasasa haupo tena.

Makalla ameyasema hayo hii leo Novemba 25, 2022 mara baada ya kutembelea chanzo cha maji Ruvu chini, na kujionea hali ilivyo ya ujazo wa maji ambao umerejea kwenye hali yake ya kawaida kufuatia mvua zilizonyesha siku za hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla (kulia), mara baada ya kutembelea chanzo cha maji Ruvu chini.

Amesema, “Vyanzo vya maji vinavyotegemewa ni Ruvu juu inayochangia lita196 milioni na hapa Ruvu chini inachangia maji lita 270 milioni na kufanya jumla kuwa lita za ujazo 466 milioni na sasa tuna maji ya kutosha.”

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kutokana na hatua zilizochukuliwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani una maji ya kutosha zaidi ya mahitaji huku akikiri changamoto ya miundombinu kuwa bado ni tatizo.

Serikali kupata asilimia 75 mafuta na gesi
Young Africans yaihofia Mbeya City, Kaze afunguka