Katika hali isiyo ya kawaida shirika la maji safi na maji taka DAWASCO jijini Dar Es Saaal na Pwani DAWASCO, limeingia mtini katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina ya kutembelea miondombinu  ya maji taka na maji safi Jinini Dar Es Salaam na Pwani Leo.

Licha ya Shirika hilo kupewa taarifa ya ziara ya Naibu waziri Mpina mwezi mmoja kabla limekaidi kwa kutoitikia wito huo hata kwa kumuwasilisha mtumishi mmoja kuwakilisha shirika hilo.

Akiongea mara baada ya kutembelea Bomba la kusafirisha maji taka kwenda baharini la Ocean road,  Mpina amesema ubovu wa bomba la ocean road unaotokana na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu, unaonyesha dhahiri kuwa DAWASCO haijalifanyia ukarabati kwa muda mrefu Bomba hilo lililoko karibu na maeneo ya ikulu.

Aidha Mh. Mpina alitembelea mabwawa ya maji taka ya mabibo na buguruni,  na alisema kuwa pamoja na miondombinu hiyo kuelemewa na wingi wa wakazi wa Dar Es Salaam, Mamlaka husika zina wajibu wa kuyafanyia usafi mabwawa hayo.

Naibu Waziri Mpina alisisitiza kuwa ubovu na uchafu wa miundombinu hiyo unapelekea uchafuzi wa mazingira na hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na viumbe hai wengine.

Kwa upande wao wana nchi wanaozunguka maeneo hayo walisema“Mabwawa hayo ni mali ya Dawasco na hata wakitaka kuunganisha maji taka kwenye mabomba yao kuelekea kwenye mabwawa wanatozwa kodi,na wenye viwanda halikadhalika wanailipa dawasco kwa kupitisha maji taka yao katika miundombinu hiyo.

Ziara ya Naibu waziri Mpina ya kukagua miundiombinu ya DAWASCO leo Jijini Dar Es Saalam ilihusisha maafisa kutoka DAWASA na Baraza la taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC na kuwaagiza NEMC, wapitie miradi yote inayosimamiwa na DAWASCO na kuona kama wanatenda haki katika kutoa huduma kwa wana nchi

Video: Jerry Muro atangaza kurudi kazini, Aiomba TFF nakala ya hukumu
Serengeti Yafungua Ukurasa Afrika Kusini, Wajue Nyota Wake