Msanii wa muziki nchini Nigeria D’banj amepata pigo mara baada ya mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja, Daniel iii aliyezaa na mke wake Didi kufariki dunia.

Vyanzo mbalimbali vimeripoti kuwa mtoto huyo amefariki dunia mara baada ya kuzama kwenye maji siku ya kuamkia jana.

Bado D’banj hajazungumza jambo lolote juu ya kifo cha mtoto wake Daniel, aidha katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram amepost picha nyeusi iliyosindikzwa na maneno yaliyosema

”Hizi ni nyakati za majaribu lakini Daima Mungu wangu ni mwema” Dbanj.

 

Mungu aipumzishe roho ya malaika Daniel iii mahali pema peponi.

Anthony Martial akaribia kutoka Old Trafford
Walionyakua tuzo za BET Awards 2018

Comments

comments