Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amewapiga marufuku wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee na Saed Kubenea kutumia ofisi zilizopo katika Manispaa ya Kinondoni.

Amesema kuwa Hakuna Sheria inayomlazimisha yeye kuwapa ofisi wabunge hao katika Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni.

Aidha, wabunge hao kabla ya kufukuzwa na mkuu wa wilaya hiyo, walikuwa wakitumia ofisi ambazo ziko chini Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Hata hivyo, wabunge hao walikuwa wakitumia ofisi hizo katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii na wananchi wao kwa ujumla

Video: Dogo Janja amwimbia Uwoya ''Wayuwayu''
Tweet ya Kikwete yazua gumzo mtandaoni