Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amepokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Maperamengi katika ziara yake kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo kilometa 130 toka Iringa mjini ambapo kilometa 70 ni pori la hifadhi na mito.

Wakati wa mvua kijiji hicho huwa hakifikiki kwa njia ya gari bali boti au mitumbwi.

Wakati wa mkutano wa hadhara, mkazi wa Maperamengi Bwana Marwa Chacha amesema kuwa kijiji hicho hakijatembelewa na Mkuu wa Wilaya toka mwaka 2010.

“Kijiji chetu mara ya mwisho kumpokea Mkuu wa wilaya ilikuwa 2010 ambapo DC Msangi alikuja, kuanzia hapo hakuna mkuu yoyote aliyewahi kufika hapa Mungu akubariki “ Amesema Marwa.

Katika ziara hiyo, Kasesela ametembelea ujenzi wa darasa ambalo mwaka jana alianzisha mchango wa kuchangia ujenzi wake. Pia ametembelea Zahanati iliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Wananchi wa Maperamengi wamelalamikia sana wingi wa wanyama hatari kama Viboko ambao wamekua wanaua wavuvi mara kwa mara na kumuomba mkuu wa wilaya serikali ivune wanyama hao ambao wamezaliana sana.

Yametimia: Mariano Díaz Mejía arejea Santiago Bernabeu
Mnada wa Makontena 20 ya Makonda watangazwa