Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewapa wiki mbili watendaji wa Kata ya Mlandege kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi ya kila mitaa.

 Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara ambapo alikuwa akisikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuona namana ya kuzipunguza.
Kasesela amesema kuwa kata ya Mlandege haina changamoto nyingi ila changamoto hizo zinasababishwa na viongozi wa Kata kwa kutofanya mikutano ya hadhara kwa wakati.
Aidha amesema kuwa ataendelea kutatua kero zote kwa wananchi kwa kuwa yeye ni kiongozi wa
wananchi na ameletwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya kazi kwa wananchi.
Kwa upande wake mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa, Ritta Kabati amesema kuwa amepokea kero na atazipeleka bungeni kutafutia ufumbuzi wa kero hizo wananhi.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Dkt. Mafwele amesema kuwa amezisikia kero zote na atazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili kuboresha maisha ya wananchi wa Manispaa ya Iringa

Abdulrahman Mussa Mchezaji Bora Wa VPL Aprili, 2017
Ligi Kuu Tanzania Bara Kuendelea Wikiendi Hii