Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewata wasanii wa filamu nchini Tanzania kujishughulisha na shughuli mbalimbali tofauti na maigizo.

Ameyasema hayo mara baada ya Wasanii wa filamu nchini Tanzania, wakiongozwa na Jacob Stephan JB, Steve Nyerere, Jack Wolper, Aunt Ezekiel na wengine wengi kuwasili Mkoani Iringa kwa ajili ya tamasha la Amka Kijana litakalofanyika Jumamosi ya leo (April 14, 2018) katika Viwanja vya Mwembe Togwa.

Amesema kuwa inasikitisha kuona tasnia ya filamu inashindwa kwenda mbele kwa kasi kubwa ambapo amewataka wasanii hao kuanza kujishughulisha na kazi nyingine nje ya sanaa zao ili kuwa na vyanzo vya mapato vya kutosha.

“Wasanii bila kufanya biashara lazima utayumba katika maisha yako, nyie wote hapa mnauwezo wa kuwa matajiri, ni jambo la kuamua tu nataka kufanya kitu fulani na mambo yakaenda,”amesema DC Kasesela

Hata hivyo, DC huyo amewataka wasanii hao kuwekeza mkoani Iringa kwa kununua mashamba na kupanda miti kwani biashara hiyo imewanufaisha wengi mkoani huyo.

Alichokisema Goodluck Gozbert baada ya kukutana na JPM
Video: Zitto atoa kauli ya kutisha bungeni, Akina baba 205 wasaini kuwajibika kwa Makonda

Comments

comments