Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon ‘Nikk wa Pili’ amewataka wananchi wa Kisarawe kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa watakapofika kwa ajili ya zoezi la kuhesabu watu na makazi.

Simon ameyasema hayo, katika Tamasha la kuhamasisha zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika hapo kesho siku ya Jumanne Agosti 23, 2022, lililofanyika Kisarawe na kuhudhuriwa na mamia ya Wananchi.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya pia amewakumbusha Wananchi kuwa zoezi hilo ni muhimu na hufanyika kila baada ya miaka 10, hivyo wajitahidi kuwa majumbani siku husika ya Sensa ili kuwasubiri Makarani.

Tamasha hilo, la kuhamasisha Sensa lilianza majira ya Saa 12 Alfajiri kwa wananchi kushiriki mbio fupi za mtaa kwa mtaa, ikifuatiwa na michezo ya soka la wanaume na wanawake na Tamasha muziki.

Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo, alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo ambapo pia lilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge.

Victor Akpan: Nilijua Simba SC kuna Presha
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 22, 2022