Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuwajibika katika shughuli za maendeleo kwa kufanya kazi kwa kushirikiana, huku wakijiiepusha kuingia kwenye makundi ya uhalifu.

Aidha, amesema kuwa uwajibikaji mzuri humsaidia mtu kukuza maendeleo yake na Serikali, hivyo wazingatie utendaji kazi katika kutimiza majukumu yao katika kujiletea maendeleo.

“Wananchi mnatakiwa kuwajibika  katika maendeleo kwani ndiyo njia pekee inayokuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla”.amesema Lyaniva.

Lyaniva amesema wakati huu wa kuelekea mwishoni mwa mwaka, kila mtanzania anatakiwa kutafakari alichofanya tangu mwaka huu uanze mpaka sasa unaisha, kama hakutimiza malengo ajipange kwaajili ya mwaka ujao.

Waliokamatwa malawi sio majasusi
Majaliwa: Ole wao watakao waachisha masomo watoto kike