Mkuu wa Wilaya (DC) ya Ilala, Sophia Mjema ametoa ufafanuzi wa kauli yake kuhusu kuzuia watu kufanya ibada katikati ya juma akidai kuwa hawezi kuzuia watu kufanya ibada kwenye siku hizo ila anawataka wamiliki wa makanisa kufuata sheria ya kusajili makanisa hayo.

Kauli hiyo aliitoa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es, Makonda kutengua agizo lake na kuwataka viongozi kuwa makini na kauli zao.

Katika ziara yake kata ya Mchafukoge, Mjema amesema hawezi kuzuia watu kuabudu na anachokifanya ni kukagua miradi ya maendeleo, ikiwemo uchafuzi wa mazingira, kelele baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi.

Amesema kuwa wao kama viongozi ni wajibu wao kusikiliza wananchi pande zote ambao wengine hufika ofisini kwake na kulalamika suala la baadhi ya makanisa yanayoanzishwa bila kufuata sheria na kuweka maspika usiku kucha, huku wakiomba na kuleta usumbufu kwa watu wengine.

”Pia ziara yangu naangalia suala la uchafuzi wa hewa na uchafuzi wa kelele, wananchi wamekuwa wakija na kulalamika kwamba mkuu tumekuwa tukienda kulala lakini makelele, wanafunga spika zao na kupiga kelele, kwa hiyo ndiyo maana ziara hizi tumekuja kuwasikiliza hukuhuku na wananchi hao wote ni wetu.

Narudia tena, wale ambao wako kwenye makanisa ambayo hayako rasmi  kwa sababu makanisa mengine hayako rasmi kwa sababu makanisa yapo yanasali siku zingine za katikati ya wiki wanaendelea kwa mujibu wa taratibu na sheria hayo yanaendelea kama kawaida.

Lakini wale ambao wamejenga tu turubai halafu wameanzisha pale kwa kuweka maspika hao lazima watuambie je wameshasajiliwa

Amesema tayari ameshazungumza na Ofisa Utamaduni akaone kama wamesajili na wanafuata taratibu kwa sababu tunachoka ni kila Mtanzania aishi vizuri na wote waheshimiane, kwa wale wanaohubiri na wale wanaosikiliza.

”Nataka kuliweka sawa kabisa, mimi ni muumini mzuri na ninamwamini Mungu, kwa hiyo siwezi kuzuia watu wasiende kuabudu” amesema Mjema.

Tumesema watu wanaweka makanisa na ukiingia unakuta kuna watu watano au sita, sasa hawa watu ndio wanaosali jumatatu hadi ijumaa, kazi wenzetu wanafanya lini amehoji mjema.

Video: Harmonize amtaja Chibu na Zari kwenye ngoma yake mpya 'Uno' sikiliza hapa
Wakurugenzi watakiwa kupambana na malaria