Mtu mmoja mkazi wa Jiji la Dar es salaam, anahofiwa kupoteza maisha baada ya kuzama katika bonde la mto Msimbazi maeneo ya Jangwani.

Imeelezwa kuwa mtu huyo alikuwa katika shughuli zake za Kuokota chupa za plastic katika mtohuo.

Mkuu wa Wilaya ya  Ilala, Sophia Mjema ameshirikiana na  Wananchi kumtafuta na amewataka wakazi wa Jiji kuwa waangalifu ili wasipatwe na madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mjema amesema licha ya kuwa jitihada za kumtafuta mkazi huyo hazijazaa matunda, vikosi vya uokoaji vinaendelea kumtafuta.

Aidha amesisitiza ” Tusiwe tunasema haya maji ni kidogo Mimi Ni mzoefu, unaweza ukaingiza mguu, tope likakukamata maji yakiendelea kuja Huna ujanja, kitakachotokea Ni Kama kilichomtokea huyu mwenzetu”

 

Video: Professor Jay "Siuelewi ugomvi wa Alikiba na Diamond"
Usiyoyajua juu ya maisha ya Mende 'Anaweza kuishi bila kichwa'