Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema amegoma kupokea mradi wa maji katika Kata ya Kitunda kwasababu ya kutoridhishwa na mradi wa ujenzi huo.

Mjema ameukataa mradi huo wakati wa ziara ya kutatua kero za wananchi katika Kata zote za Ilala, na kusema hajaona alichokuwa anategemea kukipata katika mradi huo ambao serikali imetoa jumla ya millioni 50 lakini mradi haufanani na pesa iliyotolewa.

Amesema kuwa hataki kuona watu wanatumia pesa ya miradi ya wananchi kwa ajili ya manufaa yao, na kama wapo wanaofanya hivyo basi watambue kuwa wamefeli.

“Kuanzia leo naomba huo mradi ubadilishwe ili uwe na thamani ya milioni 50 na nitakaporudi tena nataka nikute uzio katika mradi, ngazi ya kupanda juu kwa ajili ya kusafisha tenki, walinzi wawepo kwa ajili ya ulinzi pia maji yawekewe dawa,” amesema Mjema.

Hata hivyo, Mjema amewataka wanawake, vijana na walemavu kuchangamkia fursa ya mikopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha na kuepusha wimbi la watu wasio na kazi mtaani.

 

Twaweza yakanusha mkurugenzi wake kuwa mwanachama wa Chadema
Wanajeshi wagoma, wafyatua risasi juu kwa saa nne