Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameitaka Manispaa ya Ilala kuweka mageti katika barabara ili kudhibiti na kuzuia magari yenye uzito mkubwa kutumia barabara zinazotengenezwa  kwa uzito maalum.

Ameyasema hayo wakati wa makubaliano ya uwekaji saini kati ya Manispaa ya Ilala na Kampuni ya kutoka Nchini China kwaajili ya ujenzi wa barabara tano za awamu ya kwanza.

Amesema kuwa nchi za wenzetu huweka mageti kulingana na ukubwa wa gari linalotakiwa kupita katika barabara husika hali inayowalazimisha wenye magari kufuata masharti.

“Polisi ni binadamu hawawezi kuwa kila mahali sasa nawaagiza wekeni mageti kulingana na ukubwa wa gari zinazotakiwa kupita katika barabara hizo ili kudhibiti uharibifu”amesema Mjema.

Aidha, Mjema amewataka  wafanyakazi hao kufanya kazi kwa kasi kubwa kwa mwaka 2017 kwakuwa Serikali ya awamu ya tano ni ya mchaka mchaka.

Ubize wa wazazi huchangia kuporomoka kwa maadili ya watoto
Serikali yatoa onyo kuzungumzia Faru John