Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara, Chelestino Mofuga amesimamia zoezi la kuteketezwa kwa moto kwa nyumba sita wilayani humo baada ya wamiliki wa nyumba hizo kukaidi agizo la serikali la kuondoka ndani ya siku saba katika maeneo ya hifadhi.

Aidha, Miongoni mwa nyumba zilizoteketezwa kwa moto ni pamoja na nyumba ya Diwani wa Kata ya Eshkesh, Rumay Ologa ambaye baada ya kupata taarifa hizo alijisalimisha Kituo cha Polisi cha Hydom.

Akizungumza wakati zoezi hilo likiendea, Mofuga amesema kuwa njia hiyo itasaidia kuinusuru hifadhi hiyo na kukomesha tabia ya uvamizi wa hifadhi.

“Nawataka wavamizi wote wa maeneo ya hifadhi yetu iliyopo Mbulu kuhama kwa hiari yao ndani ya siku saba, kwani taarifa wanazo lakini wanakaidi,” amesema Mofuga.

Hata hivyo, pamoja na mambo mengine, Mofuga amesema kuwa operesheni ya kuwaondoa wavamizi hao kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Jeshi la Polisi, watu hao baada ya kuchomewa nyumba zao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kuwapeleka mahakamani.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 27, 2018
Dkt. Kigwangalla awawashia moto waliovamia Pori la Akiba