Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amemuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija alieteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli, ambapo amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za serikali.

Aidha amewataka wahakikishe wanaboresha mazingira ya uwekezaji huku akiwataka watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kwa pamoja watatue kero za wananchi.

Pia amewahimiza Wakuu wa Wilaya kusimamia ulinzi, usalama na amani hususani kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ludigija ameeleza kuwa ataenda kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.

Wanachuo kuendeleza urithi wa utamaduni
Rais Magufuli apewa tuzo ya heshima