Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli, kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi mbalimbali za uongozi ambapo amewamba watendaji wenzake wapya kumpa ushirikiano.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais Magufuli amteue kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, kutoka katika nafasi ya Ukurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.

“Nimshukuru sana Rais kwa kuendelea kuniamini, tumekuwa hapo Manispaa ya Kigamboni tumefanya mambo makubwa lakini kwa jukumu hili jipya ni jukumu kubwa na Ilala ni wilaya ya kibiashara na wananchi wengi wanategemea sana Ilala niwaombe watumishi wa Ilala kunipatia ushirikiano ili tuhakikishe kwamba tunawatumikia wananchi wetu” amesema Ludigija.

“Niseme kwamba mimi ni mtu ambaye napenda sana kutembea Site nijue eneo ambalo nalisimamia lakini pia nitahakikisha napata muda wa kuwa ofisini ili niweze kuwahudumia makundi yote wale wenye shida ya mtu mmoja mmoja nao watapata kuhudumiwa”.amesema Ludigija

Mwanaharakati nguli Hong Kong akamatwa
Waziri Mkuu ampa Prof. Ndalichako asiku saba