Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amemtaka mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Oscar Ng’itu kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wenye tabia ya kutuma wawakilishi kwenye vikao muhimu baada ya kubaini kuwepo kwa tabia hiyo inayopelekea baadhi ya hoja kukosa ufafanuzi wakati wa Vikao na Ziara mbalimbali za Viongozi jambo ambalo pia ni kinyume na sheria za Utumishi wa Umma.

Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo hivi karibuni alipokua katika kikao baina yake na Watendaji wa Kata na Vijiji Halmashauri ya Mji Nanyamba, Kikao ambacho pia kilihudhuriwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni, Afisa Tawala, Saidi Yasini pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Oscar Ng’itu.

Katika kikao hicho mkuu wa wilaya alidai kuwa alitoa taarifa kwa mkurugenzi kumtaka kuwaita watendaji wote wa Kata na Vijiji kwa ajili ya kuzungumza nao juu ya changamoto mbalimbali pamoja na kutoa miongozo/Maagizo ya kiutendaji lakini kilicho mshangaza ni kuona baadhi ya watendaji wamepuuza agizo hilo.

“Nikutake mkurugenzi uchukue majina ya watendaji wote ambao hawajahudhuria katika kikao hiki kisha wataarifu wanipe maelezo kwanini wameshindwa kufika, hii haikubaliki haiwezekani watu wanataarifa na kwa makusudi wanajua nataka kutoa maagizo Gani?”.Amehoji Mmanda

Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Mji wa Nanyamba, Oscar Ng’itu amesema kuwa amepokea maagizo hayo ya mkuu wa wilaya na kuahidi atawachukulia hatua watendaji hao hata kabla ya kupeleka majina yao kwa mkuu wa wilaya.

Awali kabla ya mkuu wa wilaya kutoa maagizo hayo kwa Katibu tawala wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni aledcf iliwataka watendaji hao kuzingatia miongozo na sheria za Utumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kutekeleza maagizo mbalimbali yanayo tolewa na serikali.

Hata hivyo, katika kikao hicho mkuu wa wilaya amewataka watendaji hao kuweka kipaumbele uhamasishaji wa wananchi kuitikia wito wa serikali wa kuchukua vitambulisho vya wajasiliamali kwa wale wenye sifa , ambao ni wafanyabiashara wenye kipato cha Mauzo ghafi yasiyo zidi shilingi Milioni nne (4) kwa mwaka.

Marekani yatoa zawadi ya mabilioni kumnasa mtoto wa Osama
Mbowe, Matiko washinda Rufaa kuhusu dhamana