Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameomba msaada wa kujengwa kwa choo kipya katika shule ya msingi Selian ambayo hivi karibuni ilisababisha watoto 65 kunusurika kifo baada ya choo cha shule hiyo kubomoka.

Amesema kuwa zoezi la uokoaji limeshakamilika na sasa anaomba msaada wa milioni 25 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa choo kipya kwa ajili ya wanafunzi hao.

“Tunaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya choo kwa watoto wetu, tumeazimia kujenga choo aina ya Swashi, ambacho hakitakuwa na shimo katika eneo la maliwato na badala yake shimo litajengwa pembeni Kabisa ya choo.”amesema Muro

Aidha, Muro ameongeza kuwa gharama zinaonyesha ni shilingi milioni 25 ambazo zitajenga choo cha matundu 20, na anaomba michango ya vifaa, michango ya fedha na michango ya nguvu kazi kusaidiana hata kama sio makzi wa Arumeru.

Hata hivyo, Muro ameelekeza kufuatwa kwa vigezo maalum vya ujenzi wa choo kama inavyotakiwa na ramani za halmashauri ili kuepuka maafa ya mara kwa mara.

Kocha wa Uingereza azimia ghafla
Video: Ronaldo azidi kung'arisha Juventus