Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jery Murro ametoa mwezi mmoja kwa wanaume waliotelekeza watoto wilayani humo kuhakikisha wanaanza kutafuta watoto wao na kuanza kuwahudumia .
 
Amesema kuwa baada ya muda alioutoa kuisha ataanza kuwakaribisha Wanawake wote wanaoishi wilayani humo waliotelekezewa watoto kupeleka Malalamiko yap ofisini kwake.
 
Aidha, ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya utelekezji wa watoto wilayani humo.
 
Vile vile ameongeza kuwa lengo la zoezi hilo ni kupunguza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ,hatarishi na wanaojihusisha na uhalifu na wale wanaozurura na kuzagaa mitaani kwa kukosa malezi ya wazazi wawili.
 
“Nichukue fursa hii kuwataarifu akinamama na akinadada waliozalishwa na kutelekezewa watoto na kuachwa wabebe Mzigo wa kuwahudumia watoto wao, Natoa mwezi mmoja kwa kila mwanaume anayejua ana mtoto Arumeru, aanze kuhudumia, amesema DC Murro
 
  • IGP Sirro: Kwasasa moto wetu ni mkali
  • Rungwe ‘aamsha’ na waliohama vyama, atabiri ya 2020
  • Kangi Lugola aagiza kukamatwa kwa wanafunzi watoro
 
Hata hivyo, Muro amesema licha ya serikali kutangaza elimu bure kwa wanafunzi, wapo baadhi ya wanafunzi ambao wanakwenda shule bila sare ya shule, madaftari au viatu huku moja ya sababu inayochangia hali hiyo ikiwa ni kutelekezwa na baba zako
Marekani yadai China inajiandaa kuishambulia kijeshi
Chadema yateua watakao gombea, Ukonga,Korogwe na Monduli